1.Usiku mtakatifu!
Wengine walala
wakeshao ni Yosefu
tu na Maria waliomlinda
Yesu mwana mzuri x2
2. Usiku mtakatifu!
Wachunga wapewa
habari nzuri na malaika,
zienezwe popote sasa:
Yesu mponya kaja x2
3. Usiku mtakatifu!
Siku ya furaha
imetuangaza Kimungu
tumeupewa ukombozi
Kristo amefika x2